burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

1 Jan 2018

Manchester City wapata pigo


Mshambuliaji machachari wa Manchester City, Gabriel Jesus atakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na jeraha alilopata wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace Jumapili ambapo walitoka sare 0-0, meneja Pep Guardiola amethibitisha hilo.

Mbrazil huyo wa miaka 20 alionekana kuumia kwenye goti kipindi cha kwanza wakati wa mechi hiyo uwanjani Selhurst Park.

Aliondolewa uwanjani akitokwa na machozi.

Kiungo wao Kevin de Bruyne pia huenda akakosa kuwachezea kwa muda baada ya kuondoka uwanjani akiwa amebebwa kwa machela.

Mbelgiji huyo hata hivyo alionekana nje ya uwanja baada ya mechi, dalili kwamba huenda hakuumia sana.

“Nafikiri Gabriel atakuwa nje kwa mwezi mmoja hivi au siku chache zaidi, naye Kevin tutasubiri Jumatatu tujue iwapo aligongwa tu kidogo au ameumia sana,” alisema Guardiola.

Msimamo wa ligi ya EPL 2017/18
Guardiola: Manchester City hawatamaliza ligi bila kushindwa
“Ni lazima ukubali ukali na ugumu wa ukabaji Ligi ya Premia, lakini waamuzi wanahitaji kuwalinda wachezaji, hilo ndilo naomba pekee.”

Jesus atakosa mechi dhidi ya Watford Jumane.

De Bruyne naye ambaye ameng’aa sana msimu huu na kusaidia ufungaji wa mabao tisa Ligi ya Premia msimu huu aliumia baada ya kukabiliwa na kiungo wa Palace, Jason Puncheon.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni