burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

3 Mac 2018

Nay kuachia remix ya wimbo ‘Mikono Juu’ baada ya wimbo huo kufungiwa


Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amewataka mashabiki wake wa muziki nchini kusubiria remix ya wimbo ‘Mikono Juu’ ambao umefungiwa na Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza kwa kigezo cha maadili.

Rapa huyo mchana huu amewauliza mashabiki wake kama aachie remix ya wimbo huo au la!.

“Unadhani Tuachie Goma Lingine Au Tuache #MikonoJuu Iendelee Au Tufanye Remix,” aliandika Nay wa Mitego kupitia facebook.

Baada ya post hiyo mashabiki walionesha kuhitaji remix hiyo ndipo alipowaahidi mashabiki kwamba ataachia remix hiyo kwaajili ya mashabiki wake.

Rapa huyo mapema jana alidai kama angefungiwa na BASATA basi angeachana na kazi ya muziki na kujikita katika biashara zake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni