burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

1 Nov 2017

Nyomi la mashabiki la kwamisha mazoezi Al Ahly


Timu ya Al Ahly ya Misri hapo jana imeshindwa kufanya mazoezi katika makao makuu ya klabu hiyo huko Cairo baada ya mashabiki kujaa Uwanjani.

Mamia ya mashabiki waliingia Uwanjani kuitazama timu hiyo hali iliyosababisha wachezaji kushindwa kufanya mazoezi na hivyo kughairishwa.

Wamisri wanatazamia kuweka rekodi ya kutwaa kombe la Afrika mara ya tisa endapo wataifunga timu ya Wydad Casablanca siku ya Jumamosi huko Morocco.

Katika mchezo wa awali uliyofanyika Alexandria timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Ahly itahitaji kufanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wao wa nyumbani kabla ya kusafiri siku ya Jumatano kuifuata Wydad Casablanca huko Morocco.

Ahly wamekutana na klabu hiyo ya Afrika Kaskazini 2006 kwenye mechi ya CAF Super Cup.


Timu hizo zimekutana mara nne kwenye michuano hii awali. Wydad wakiing’ang’ania Ahly kwa sare ya 3-3 mnamo 2011 mjini Cairo na 1-1 mjini Casablanca na 2016 sare ya bila kufungana mjini Alexandria na hatimaye Ahly kushinda 1-0 Morocco, kabla kukutana tena na nakutoka sare ya 1-1 Alexandria mwaka huu.

Msimu huu timu zote zilikuwa kwenye kundi moja, kila moja ikishinda 2-0.

Al Ahly ambao wanatafuta ubingwa wa tisa, waliifunga Etoile du Sahel 7-2 nyumbani na ugenini kutinga fainali.



Licha ya kupata kipigo  cha 2-1 Sousse, Mashetani Wekundu walibadilika katika ardhi ya nyumbani kwao Misri na kushinda 6-2. Walid Azaro akifunga hat-trick kwa timu hiyo ikiwa nyumbani.

Kwa upande wa Wydad, walishinda 3-1 mjini Casablanca baada ya sare waliyopata mjini Algers dhidi ya USM Alger, katika harakati zao za kutwaa ubingwa wa pili Ligi ya Mabingwa tangu waliposhinda 1992.

Mshindi atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani milioni 2.5 na atapata tiketi kuiwakilisha Afrika kwenye michuano ya klabu bingwa duniani mwezi Disemba falme za kiarabu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni