Msanii wa muziki anayefanya vizuri na wimbo ‘Lover Boy’ Barnaba Classic amesema amelazimika kusitisha kuachia albamu yake mpya na kujipa muda zaidi wa kujipanga.
Muimbaji huyo ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki wa High Table Sound, alipanga kuachia albamu hiyo Agosti 8 mwaka huu. Barnaba alisema amesitisha kuachia albamu hiyo baada ya kuona kuna baadhi ya vitu havijakamilika.
“Kila kitu kina mpango wake, nimeangalia wakati haupo sawa, nimeona kuna mambo ambayo hayapo sawa,” alisema Barnaba. “Lakini mashabiki wangu wasijali mpango upo pale pale tena kuna mambo mazuri zaidi yanakuja na sio kwa ubaya”
Aliongeza, “Ndio maana kwenye ‘Lover Boy’ kama nimewajaribu vile kuona kama kile nilichokiandaa kwenye albamu kipo sawa, na mapokezi yamenionyesha ni jinsi gani nimeandaa mambo makali kwenye albamu, kwahiyo muda ukifika albamu itatoka tu,”
Muimbaji huyo amesema atatangaza muda wowote ni lini albamu hiyo itatoka ili kwenda kukata kiu ya mashabiki wake.
Jiunge na g.loveTZ.com sasa
Gusa HAPA kwa kumjua zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni