Msanii wa muziki, Bob Junior amesema yeye ni rapa mzuri hivyo anajipanga kuachia wimbo mmoja ili kuonyesha uwezo wake wa kuchana.
“Unajua mimi ni Rapa hivyo mwaka huu nitaachia kazi yangu mpya ya kuimba ambayo itakuwa na ‘Sound’ mpya kabisa kutoka Sharobaro Records lakini pia nitaachia kazi yangu nyingine ambayo nimechana mwanzo mwisho” Bob Junior alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Siachaninae’ aliomshirikisha msanii wa Uganda, Jose Chameleone.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni