Samsung imetoa angalizo kwa wateja wake Jumatatu hii ikiwataka wazizime simu zao Galaxy Note 7 ambazo zimekuwa zikishika moto.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Samsung kusitisha utengenezaji wa simu hizo hatari kwa maisha ya watumiaji.
Kwenye maelezo yake rasmi, Samsung imesema itayaomba makampuni na mawakala wake duniani kote kuacha mauzo ya Galaxy Note 7, wakati inachunguza chanzo cha kushika moto.
Imewaomba pia wateja wenye simu za awali za Galaxy Note 7 au zile walizobadilishiwa, kuzizima na kuacha kuzitumia kabisa. Hatua hiyo imekuwa na matokeo hasi kibiashara kwa kampuni hiyo ya Korea Kusini. Hisa zake Jumanne hii zimeshuka kwa asilimia 5 mjini Seoul.
Mapema September, Samsung ilizirudisha kiwandani simu milioni 2.5 kutoka duniani kote na kuanza kutoa simu mpya kufidia, ambazo nazo zimegundulika kuwa na tatizo la kushika moto.
Jumatano iliyopita, moshi ulianza kutoka kwenye Galaxy Note 7 mpya kwenye ndege ya Southwest Airline kabla haijapaa na kulazimika kusitishwa kwa safari.
G.LOVETZ.BLOGSPOT.COM
kama ulipitwa na video ya G.LOVE-TUKO PAMOJA hii apa
kwa kuitazama gusa HAPA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni