Diamond Platnumz na Ne-Yo wameunganisha nguvu ya pamoja kuishambulia Uingereza. Wawili hao watakuwa na ziara ya pamoja mwezi Disemba mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia akaunti ya Instagram ya Revolt Africa.
“Africa & America join forces!! @DiamondPlatnumz & @Neyo UK tour this December! The movement continues… #AfricaToTheWorld #MusicToTheWorld #Neyo #neyonation #diamondplatnumz #rnbking #rnb #Tanzania #africa #afropop #afrornb #afrobeatsuk #afrobeats #afrobeat #kidogo #wcb #revolttvafrica #afroBeHeard,” wameandika.
Wakali hao wenye wimbo wa pamoja uitwao Marry You, watafanya show sita kwenye majiji mbalimbali nchini humo. Mara ya kwanza Diamond aliongelea ujio wa ziara yao kupitia mahojiano aliyofanya kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM Jumamosi iliyopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni