Msanii wa kike mwenye sauti ya dhahabu kwenye Bongo Fleva, Ruby ameongeza idadi ya wasanii kutoka Tanzania wanaoshiriki kwenye kipindi cha Coke Studio Africa Season 4.
Huu ni msimu wa kwanza kwa Ruby kushiriki kwenye kipindi hicho ambapo ameungana na msanii wa Nigeria, Yemi Alade kutengeneza mchanganyiko wa nyimbo zao tofauti tofauti.
Wasanii wengine wa Tanzania walioshiriki kwenye kipindi hicho kwa msimu huu wanne ni pamoja na Joh Makini, Vanessa Mdee, Yamoto Band na Diamond aliyeshiriki Coke Studio Za. Tazama video hapa chini.
Jiunge na g.loveTZ.com sasa
Gusa HAPA kwa kumjua zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni