Kundi la muziki la Navy Kenzo linaloundwa na wasanii wawili, Aika na Nahreel wamesema lengo la kundi lao kwa sasa ni kwenda kwenye chart kubwa za muziki duniani Billboard pamoja na kwenye tuzo za Grammy.
Kundi la Nany Kenzo limekuwa nominated kwenye tuzo za MTV Africa Music Awards ambazo zitafanyika Afrika Kusini Octoba 22 mwaka huu.
Akiongea katika kipindi cha The Playlist cha Times FM Jumamosi hii, Navy Kenzo wamesema tayari kwa sasa wanakolabo za kutosha na wasanii wa Afrika ambazo zitawatangaza vizuri Afrika.
“Tutegemee kolabo zaidi na wasanii wakubwa duniani, ndoto yetu mwaka huu ni kwenda Billboard, kwenda Grammy na kufanya vitu vikubwa zaidi, kwa hiyo tunashukuru Mungu connetion zinazidi kuwa kubwa,” alisema Aika.
G.LOVETZ.BLOGSPOT.COM
kama ulipitwa na video ya G.LOVE-TUKO PAMOJA hii apa
kwa kuitazama gusa HAPA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni