Rapper wa kike Bongo, Chemical amefunguka kwa kuelezea sababu inayomfanya afanye kazi nyingi na mtayarishaji wa muziki Maximizer.
Akiongea na mtangazaji wa Radio Maisha ya Dodoma, Silver Touchez kwenye kipindi cha Flavour Express, rapper huyo amesema Max amekuwa akimpatia kwenye beat zake.
“Nina nyimbo nimefanya na maproducer wengine lakini nafanya nyimbo nyingi na Maximizer kwa kuwa tumetoka pamoja kwahiyo nikienda naye mimi nakuwa nasimama na Max naye anasimama na pia ni mtu ambaye ananipatia sana. Ninaweza nikaenda kufanya kazi sehemu nyingine lakini nikiwa na Max nakuwa poa,” amesema Chemical.
Rapper huyo ameongeza kuwa hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na Max kama baadhi ya watu wanavyofikiria
Jiunge na g.loveTZ.com sasa
Gusa HAPA kwa kumjua zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni