Akiongea na mtangazaji wa Kings FM ya Njombe, Prince Ramalove, Fid amesema kuna watu wengi wanaoitetea hip hip na wamejipanga kuiandalia tuzo zake.
“Hip hop ni muziki unaopiganiwa na wengi wanaoipenda, ina wapenzi wake ambao huwatoi. Mwanzo ilikuwa ngumu lakini siku hizi wamekuwa wengi, waligundua wakaenda mashuleni wakasoma vizuri wakaajiriwa, wakapata nafasi nzuri za kazi kwahiyo nao wanataka kutumia position zao kusaidia,” amesema Fid.
Kwa upande mwingine Fid alizungumzia suala la Profesa Jay kufanya Singeli na kama wimbo wake unaweza kuingizwa kwenye tuzo hizo.
“Hiyo ni sanaa na hivyo ndivyo ameona yeye ni sahihi. Unapokuwa kwenye beat ya Singeli na yeye amerap, ile inakuwa ni rap song sio hip hop,” amesisitiza. “Kwahiyo kwenye tuzo za hip hop anakuwa hajaqualify, lakini yeye kama mwanahiphop anaqualify kuingia, hiyo ni aina tu nyingine ya muziki ambayo amefanya.”
Jiunge na g.loveTZ.com sasa
Gusa HAPA kwa kumjua zaidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni