Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Mwanza, Young Killer Msodoki amefunguka kwa kusema kuwa kila kukicha changamoto mpya zinajitokeza katika tasnia ya muziki.
Rapper huyo ameiambia g.loveyz kuwa wakati anaanza muziki hakukuta changamoto nyingi kama sasa, hali ambayo amewataka wasanii wapya kukaza.
“Mabadiliko ni makubwa sana, wasanii ni wengi tofauti na kipindi ambacho mimi natoka, sasa kuna wasanii wengi zaidi, kuna muziki mpya umezaliwa Singeli. Kwa hiyo muziki umekuwa wa ushindani na kila mtu anahitaji kuonekana na watu wengi kwa hiyo ndo changamoto zenyewe na huwezi kuzikimbia lakini muziki umekuwa na changamoto sana,” alisema Young Killer
Aliongeza, “Kwa hiyo sasa hivi nikukaza, yaani hakuna kitu kizuri kama kukaza kwa sababu mashabiki sasa hivi wanasupport kazi nzuri, hawaangalii wewe ni nani, kitu kibaya wanajua kabisa hiki ni kitu kibaya, kwa hiyo wanadeal na vitu vizuri. Kwa hiyo ukikaza nadhani nafasi kwa wasanii wapya zipo kinachotakiwa ni ubunifu zaidi,”
Pia rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mtafutaji’ amewataka mashabiki wake kukaa makao wa kula kwa ajili ya ujio wake mpya hivi karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni