Mchekeshaji maarufu Stan Bakora amefunguka juu ya povu lililomtoka Barakah The Prince siku kadhaa baada ya kuachia parody ya wimbo ‘Nisamehe’.
Kupitia kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Stan amesema kuwa kama asingefanya vile video ingekuwa ya kawaida tu na isingeleta maana.
Barakah ameshindwa kuelewa. Kama nisingefanya vile ile video isingeleta maana, lazima uonyeshe uhalisia. Kwani Baraka si mweusi kweli?,” amesema Stan. Stan aliendelea kwa kumtania Barakah kwa kumwambia kuwa hapa mjini [Dar es Salaam] ndio kwanza ana Christmas mbili.
Awali baada ya Stan kuachia parody hiyo, Barakah aliandika kwenye Instagram: Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo… heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni