burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

22 Mac 2017

AT adai Rama Dee amemkosea heshima Adam Juma


Msanii wa muziki AT amemchana msanii Rama Dee kwa kuwambia anapaswa awaheshimu watu waliomtangulia.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya msanii Rama Dee kusema kiwango cha ‘director’ Mkongwe Adam Juma kiko chini ya viwango katika kutayarisha na kutengeneza ‘video’ na kwamba anamtaka ajifunze kutoka kwa Hanscana kauli ambayo ilipigwa na wadau mbalimbali wa muziki.

“Imekuwa desturi kwenye nchi yetu mtu kutomuheshimu mwenzake au nguvu zake, leo unatoka unasema Adam Juma hajui ku-shoot ‘video’, wakati wewe ukipewa ile kamera hata kupiga picha huwezi kujua lakini yule mtu ndiyo amekuja muziki wa Tanzania”. AT alikiambia kipindi cha eNewz cha EATV

Aidha msanii huyo amesema wasanii ndiyo wanaongoza kwa kutokuwa na heshima, hivyo amewataka wasanii wenzake kuwa na heshima kwa watu waliowazidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni