burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

23 Mac 2017

Samatta: Tunao wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza nje


Mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji na Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta amesema Tanzania inawachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza soka nje ya Tanzania.

Samatta ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mazoezi ya timu ya Taifa katika uwanja wa Taifa.

Samatta ambaye aliyewasili usiku wa juzi kujiunga na kikosi cha Stars kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za kimataifa wiki ijayo dhidi ya Botswana Jumamosi na Burundi Jumanne, amesifu pia uteuzi wa kikosi cha Stars wa Mayanga, kwamba umezingatia makosa yaliyojitokeza kwa walimu waliomtangulia.

Jumamosi hii Samatta ataiyongoza Taifa Stars katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana katika Uwanja wa Taifa kabla ya kuwavaa Burundi Jumanne ijayo Machi 28 kwenye uwanja huo huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni