burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

23 Jul 2017

“Fahyma anichungi” Rayvanny asema haya baada ya video yake akiwa na Gigy Money kusambaa mitandaoni

"Fahyma anichungi" Rayvanny asema haya baada ya video yake akiwa na Gigy Money kusambaa mitandaoni
Huenda Rayvanny anafuata nyayo za Diamond Platnumz – hii ni baada ya video yake na Gigy Money iliposambaa mitandaoni huku wakionekana kuwa na ukaribu usio wa kiurafiki tu.

Hata hivyo magnificent huyo wa tuzo ya BET 2017 ameiambia Times Fm kuwa yeye na Gigy Money ni marafiki tu na pia mpenzi wake Fahyma anafahamu haya. Aliendelea kuongeza kuwa yeye na Fahyma hawachungani kwa hivyo hili si jambo linaloweza kumletea shida na mama wa mtoto wake. Msanii huyo alisema,

“Hawezi kuchukia, halafu pia mimi sichungwi am live my life, president of own life, so nobody anaweza akaingilia akasema usifanye hiki, so Fahyma hana noma sometimes anaweza akafanya vitu vyake mimi simuingilii.”

Hata hivyo alidai kuwa video yake na Gigy Money ilikuwa ya utani lakini wambea waliona kuineza ilikumletea utata.

“It’s just a joke, Gigy ni mshikaji wangu na ni wa Mbeya pia, namjua before hajanza mbwembwe zake na ni mtu ambaye yupo happy muda wote mimi naona anaenjoy maisha yake”.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni