burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

3 Jul 2017

Ujerumani mabingwa kombe la mabara

Tokeo la picha la Germany winner Confederation cup 2017
Jana usiku kulikuwa na fainali ya michuano ya kombe la Mabara (Confederation Cup)  nchini Urusi kati ya Mabingwa wa dunia Ujerumani dhidi Chile ambapo Ujerumani imeibuka kidedea kwa kuichapa Chile goli 1-0 na kuchukua kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia.

Goli la Ujerumani lilipatikana dakika 20 za kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wa klabu ya BorussiaDortmund, Larsi Stindl goli ambalo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo.

Kabla ya mchezo huo kulikuwa na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kati ya Mexico na Ureno ambapo Ureno iliibuka kidedea kwa kuilaza Mexico goli 2-1, magoli ya Ureno yakifungwa na Pepe na Adrien Silva huku goli la Mexico likifungwa na Luis Neto.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni