burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

3 Jul 2017

Ni vigumu kumsimamia msanii wa kike – Quick Rocka

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na bosi wa label ya Switch Music Group (SMG), Quick Rocka ameelezea ugumu wa kumsimamia msanii wa kike na ndio maana hadi sasa label hiyo haijamsaini msanii wa aina hiyo.

Quick Rocka ametaja mahusiano kama moja ya sababu zinazopelekea ugumu huo na kusema pengine member yeyote wa OMG akiwa na mpenzi ambaye ni msanii anaweza akapata nafasi katika lebo hiyo kwa kuwa wivu hautakuwepo lakini ameonya kuwa endapo watashindwana hapo ndipo ugumu unazidi.

“It very hard kumsimamia msanii wa kike coz kuna vitu vingi hasa anapoanza kuingia kwenye mahusiano, labda yeye ana mtu wake sisi tupo on tour au kuna zile usiku mnene studio, unajua ule wivu wa hapa na pale unaweza ukamzuia asi-perform vizuri katika codes,”  Quick Rocka amekiambia kipindi cha Red Capet cha Radio One.

Label ya SMG hadi sasa ina wasanii wanne waliotoka ambao ni Quick Rocka na member wa watatu wa kundi la OMG, na sasa hivi wanatamba na wimbo wao ‘Watasema’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni