burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

29 Sep 2017

Jibu la Ommy Dimpoz iwapo alimkimbiza Barakah The Prince RockStar4000


Msanii wa Bongo Flava, Ommy Dimpoz amesema si kweli kwamba yeye kuingia RockStar4000 ndio sababu ya Barakah The Prince kuondoka katika menejimenti hiyo.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa kwanza hawana beef na walifahamiana miaka mingi hivyo hawezi kujua kilichomuondoa Barakah RockStar4000.

“Kwanza mimi na yeye tunafanya muziki tofauti hakuna sehemu tunaweza kusema unaweza ukatokea mkwaruzano na tunaheshiana na ninaamini ni moja ya wasanii wenye talent kubwa hapa Tanzania,” Dimpoz ameiambia Bongo5.

“Kwa hiyo kilichomfanya aondoke RockStar siwezi kukizungumzia wala kujua nini kilitokea yeye na RockStar ndio wana majibu zaidi,” ameongeza.

Alipoulizwa iwapo RockStar4000 imepata pengo baada ya Barakah kuondoka alisema hawezi kusemea hilo au kujua kwa sababu wakati Barakah yupo RockStar4000 yeye hakuwepo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni