burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

23 Okt 2017

Irene Uwoya Afunguka na Kusema "Naombeni Mniache"


Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya ambaye ndoa yake na mchezaji mpira Ndikumana Katauti wa Rwanda iliingia katika mgogoro mzito na kupelekea kila mtu kuishi peke yake amefunguka na kuwataka watu wasimuingilie katika malezi ya mtoto wake.

Irene Uwoya ambaye alibahatika kupata mtoto mmoja na mume wake huyo kabla ya migogoro yao, ameonyesha kukasirishwa na maneno ya baadhi ya watu kusema kuwa anamlea mtoto wake huyo kizembe zembe huku wengine wakienda mbali na kumtabiria mambo mtoto huyo kutokana na makuzi yake, ndipo hapo Uwoya alipocharuka na kuwataka wasimuombee mambo ya ajabu mtoto wake.

"Wale mnaosema namlea kizembe naombeni sana mniache, namlea navyoweza mimi na mwanangu bado mdogo sana anahitaji mapenzi ya Mama.  Hakuna hata mmoja wenu amewahi kuchangia ata mia ...sipendi kuongea sababu siyo swaga zangu, mimi mpole sana ila kwa mwanangu sina masihara. Sijawahi sema kitu ila leo nimeona niseme na sitarudia tena kusema, mwenye maskio na asikie na mwenye macho aoneee! yale mambo ya laaana mnayo mtabiria mwanangu yashindwe na MUNGU awasamehe sababu hamjui mlitendalo" alisisitiza Irene Uwoya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni