burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

7 Okt 2017

Ngoja nipite njia tofauti na Wasafi – Z Anto


Msanii wa mziki Bongo, Z Anto amesema si kwamba hawezi kufanya kazi na Diamond au label ya WCB bali anataka kupita njia yake ya tofauti.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kacheze Unapochezaga’ ameeleza sababu ya kutaka hivyo ni kutokana na kuwepo kwa team katika muziki.

“Sishindwi kufanya kazi na Diamond nina uwezo na muda wowote tunaweza kufanya kazi lakini pasipo mazingira ya u-team, hiyo inawezekana,” Z Anto ameiambia Bongo5.

“Nilishawahi kuongea na moja ya viongozi wa Wasafi lakini nikaomba ngoja nipite njia tofauti na wanayopita Wasafi, nilikuwa naongea na Tale,” ameongeza.

Z Anto ameendelea kwa kusema suala la kusaini katika label ya Diamond ‘WCB’ ni kitu ambacho hajawahi kuwa na ndoto nacho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni