burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

6 Okt 2017

Wolper afunguka salamu ya Harmonize na Brown kutohudhuria Party ya Diamond


Muigizaji wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameweka wazi juu ya salamu aliyosalimiana na  ex-boyfriend wake Harmonize katika private part ya Diamond siku ya tarehe 02/10/2017.

Akiongea kupitia kU-Heard ya Clouds Fm, mrembo huyo ameeleza kuwa  jambo la yeye kumsalimiana na Harmonize halikuwa tatizo kwani salamu haikataliwa.

“Siwezi kumshangaa sasa kwa nini nimshangae, mimi siwezi kumshangaa bhana yeye si ndo kaja kunisalimia masikini, coz nilikuwa nimekaa na Aunty akaja akanisalimia sasa sijui kama salamu inakataliwa, hata ingekuwa wewe umesalimiwa ungekataa hata ingekuwa wewe ungekataa,” amesema mrembo huyo.

Pia Wolper akadai kuwa hakutokea na mpenzi wake huyo katika sherehe hiyo kwani w alikuwa anaumwa kwa takribani siku tano na kuhusu kufutwa kwa picha zake mtandao wa kijamii wa Instagram, mrembo huyo amedai hafahamu kuhusu ilo kwani hajaingia katika mtandao huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni