Msanii wa muziki nchini, Bob Junior amemtuhumu msanii wa Uganda, Jose Chameleone kuwa ndiye aliyekwamisha video ya wimbo ‘Siachani Naye’ aliyomshirikisha msanii huyo isifanyike.
Bob Junior alidai kuwa alikuwa na nia ya kufanya video ya wimbo huo lakini kila alipokuwa anapanga ratiba za ku’shoot, Chameleone alikuwa akikwepa.
“Tukipanga siku ya ku’shoot, ikifika siku hiyo nikimtafuta basi hajibu meseji zangu, sasa mimi nitafanyaje? Hata hivyo sitaki kusema mengi kwa ubaya, labda kuna vitu kweli vinamzuia,” Bob Junior alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.
Hata hivyo Bob Junior alisema baada ya kushindwa kufanikisha kufanya video hiyo, sasa anajipanga kwa kazi nyingine, huku akisema anatarajia kuachia wimbo alioshirikiana na Q Chief na Baraka da Prince.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni