Diamond Platnumz alitosa kusainishwa na label inayomilikiwa na Jay Z, Roc Nation.
Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, staa huyo alisema hiyo ni moja tu ya label kubwa za Marekani alizozitolea nje. “Wakati nipo BET, Roc Nation walinifuata wakitaka wanisaini,” alisema Diamond.
“Acha Roc Nation kuna baadhi ya record label nyingi sana kubwa, nyingi sana, tena hawanifuati hivi hivi, wananifuata na ofa,” aliongeza.
“Lakini kila kitu ni target, mimi siku yoyote ukisikia nimefanya kazi na label kubwa duniani, sio kuwa under record label, ila pointi yangu itakuwa kwamba kuona namna gani wanaweza kukuza muziki wangu kidunia zaidi, nitafanya kila kitu mwenyewe. Kupata collabo na msanii yeyote mimi naweza kupata sababu Kimarekani collabo sio story, hela yako, ni biashara, mtu hawezi akakupa bure mfanye nyimbo ili upate hela, ukanye show yeye anafaidika na nini?”
Kingine Diamond alisema kama ni msanii mkubwa inakuwa rahisi kupata collabo za aina hiyo.
“Nataka mtu akinisaini, nataka muziki wangu uuzike kama wanavyouza akina Jay Z, Kanye West. Sitoingia eti Diamond kaingia na record label fulani, WCB itaingia na kampuni fulani na ikiingia ni katika makubaliano ya kuuza muziki katika digital kuona ni namna gani muziki wangu utauza sehemu fulani kwa bei nzuri.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni