Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Tunda Man amesema kolabo ambayo inakuja kutoka kwake ni ile aliyofanya na msanii wa Kenya, Jaguar.
Muimbaji huyo ameiambia g.lovetz kuwa ana kolabo nyingi ambazo amefanya na wasanii mbalimbali lakini kolabo ambayo amepanga kuitoa hivi karibini ni ile aliyofanya na Jaguar.
“Kuna kolabo nyingi ambazo nimefanya na wasanii wa hapa pamoja na nje lakini kolabo ambayo mpaka sasa ipo kwenye mpango wa kutoka ni kolabo ambayo nimefanya na Jaguar, kwa hiyo mashabiki watulie kuna mambo mazuri yanakuja kutoka kwa Tunda Man,” alisema Tunda.
Pia muimbaji huyo amesema bado hajajua ni wimbo upi utaanza kutoka kati ya ‘Mwanaume Suruali’ pamoja na wimbo wa hiyo kolabo yake na Jaguar.
Wimbo wa ‘Mwanaume Suruali’ ameshindwa kuuachia hivi karibuni baada ya video ya wimbo huo kuzuiliwa kutokana na kumtumia video queen ambaye ni mke wa mtu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni