burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Ago 2017

ASLAY BAADA YA ‘LIKIZO’ AJITOKEZA KAMA SIMBA


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Aslay baada ya kuzungumziwa sana kwa kasi yake ya kuachia nyimbo baada ya nyingine bila kuwaachia nafasi ya mashabiki kupumua, amedondosha nyingine ambayo mara hii iko katika maadhi na muonekana kama SIMBA.

Imani ya Rastafarian ni ya jamii ya Jamaica ambayo ndo muonekana wa ngoma mpaka miondoko yake, Aslay ameachia wimbo wake mwingine alioupatia jina la ‘Pusha’ uliyoko katika maadhi ya Reggae na katika kuweka msisitizo zaidi alivyoonekana unaweza kumuita Rastaman.

Hata hivyo kwa mahesabu ya haraka haraka ndani ya muda usiopungua miezi minne Aslay ameachia nyimbo zisizopungua sita ambazo zimetoka sambamba na video bila kujali kuwa ataweka msongamano wa nyimbo nyingi katika mzunguko wa uchezwaji katika vituo vya matangazo ndani na nje ya Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni