burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Ago 2017

BAISA MHELA AWAONYA WAIMBAJI WANAOKATA TAMAA

Image result for BAISA MHELA
BAISA MHELA  akizungumza na G,LOVETZ  amesema waimbaji wengi wanaochipukia wanakosa nguvu za kufanya huduma hiyo kutokana na sababu mbali mbali lakini ukitazama sababu zote ukizitazama ni sababisho la shetani kuzuia huduma ya Mungu kufika mbali sana  Ndivo alivoanza kusema Baisa Mhela

Mwimbaji Wa music Wa injili ambaye anakuja kwa kasi nchini Tanzania
Aliendelea kusema ukitazama sababu kubwa zinazowafanya watu kukata tamaa
Ni ghalama za studio
Ghalama za nauli
Na mengineyo kama mavazi kukatishwa tamaa na watu wanaowazunguka
Akaonya kwa kusema Waimbaji wanapaswa kujielewa kwamba wanafanya kazi ya Mungu na kikubwa na Mungu wetu ni tajili hakosi kitu wala hashindwi kitu hivo wakiomba kwa mwenye kazi yake hatawanyima

Aliongeza kwa kusema biblia inaeleza kabisa jinsi yesu alipowauliza wanafunzi wake kwamba JE MLIPUNGUKIWA NA KITU NILIPOWATUMA BILA KITU BILA MKATE BILA MAVAZI NA WANAFUNZI WALIJIBU HAPANA
Maana yake Mungu anapokutumia anakutumia kutangaza neno lake kama ulivo na hatokuacha atakulisha atakulipia na atakujaza na yote baada ya kuona hekima yako.
Aliwaaonya waimbaji wote na wainjilist mitume na manabii kutovaa sana ubinadamu Wa kulaumu au kulalamika bali wayapokee yote kama razalo mtumishi Wa Mungu katika bibilia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni