burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

6 Ago 2017

Ruge na Paul Makonda Wanapataneje na vipi Nyasi zilizoumia?


Wanajamvi salamu mbele!
Nimeona katika mtandao wa YouTube kile kinachoitwa kupatanishwa kwa Makonda na Ruge na mpatanishaji akiwa ni Rais John Pombe Magufuli. Naomba niweke maoni yangu hapa Jf na maoni haya yasitafsiriwe kuwa ninapinga watu kupatana wala kuishi kwa amani zaidi kushirikiana.

Makonda na Ruge wamekuwa katika mtanziko na hali ya kutokuelewana kwa muda wa miezi kadhaa sasa chanzo kikubwa kikiwa ni kile kinachodaiwa kwamba Makonda alivamia kituo cha utangazaji cha clouds tv na kupora vifaa kadhaa vya ofisi. Makonda alikwisha kanusha kuvamia clouds media katika kipindi chake alichojiandalia StarTv na kudai kwamba yote aliyoyaongea Ruge ni uongo ametunga akaenda mbali zaidi kusema Ruge hajui kitu zaidi ya utunzi wa story za mapenzi (kifupi msanii).

Wahenga wanasema mafahari wawili wagombanapo ziumiazo ni nyasi katika vita hii nyasi hazikukosekana. Mh Waziri Nape Mnauye ni mmojawapo katika juhudi za kutafuta ukweli na pengine suluhu la swala la Clouds media na Makonda yalimkuta ya kumkuta akaumia.
Kuna vyombo mbalimbali vya habari, watu binafsi na taasisi zingine ambazo kwa kweli zilisikitishwa na na kitendo cha Makonda kuvamia kituo cha Clouds media na wakatoa msaada wa kulaani na zaidi vilisusia kuandika habari za Makonda na mbali na vitisho vilivyotolewa na Rais ( refer "watch it")

Kubwa zaidi ni TEF (Jukwaa la Wahariri) lilisimama kidete katika hili kuhakikisha haki inatendeka kwa clouds media.

Jambo Kubwa la kunote wakati yote haya yanatokea mpatanishi (Rais Magufuli) aliamua kuegemea upande mmoja hii haijawahi kuwa sifa ya msuluhishi mahali popote pale duniani. Msuluhishi anatakiwa kuwa impartial asiyeegemea upande wowote.

Magufuli alikwishatamka hadharani kwamba kinachoendelea kwenye mitandao (tuhuma dhidi ya Makonda) ni udaku na yeye hasikilizi udaku. Hakuishia hapo alienda mbele zaidi na kutangaza interest kuwa hatamtumbua Makonda wala hata fanya lolote lile. Kauli kama hii inadhihirisha alikubaliana na alichokifanya Makonda na wala hakua akijali lolote na huku ni kuegemea upande mmoja.

Leo hii Mbele ya hadhara mlolongo huu wa matukio unamalizwa kwa kushikana mikono watu wawili yaani Ruge na Makonda? Kweli kabisa bila maelezo yoyote?

Mpaka naandika haya kuna mambo yameishughulisha akili yangu kama ifuatavyo.

Kwanza, Rais Magufuli katika mgogoro huu hakupaswa kuwa msuluhishi kwani alishaonesha upande hii inayofanywa ni danganya toto kwa Ruge.

Pili, swala hili lilipaswa sasa lisiwe mikononi mwa Clouds media na Ruge tena maana lilikwishafika kwenye chombo kinachohusika na vyombo vya habari TEF.

Tatu, Ni lazima umma uambiwe wanachopatana Ruge na Makonda ni nini ni ishu ya uvamizi au walikwaruzana mambo mengine barabarani? Na kama ni ishu ya uvamizi lazima tujue kwanza ukweli ni nani mkosaji ambaye anaomba radhi ili asamehewe? Je wanasameheana kwamba walikoseana Ruge alikosa nini na Makonda alikosa nini? Isijekuwa anayesamehewa ni Ruge kwa kumsingizia Makonda.

Je kuanzia sasa Clouds media wataanza kurusha habari za Makonda vipi kuhusu TEF na washirika wao?.
Vipi kuhusu Nape Mnauye? Na wengine walioumia kama nyasi remedy yao ni ipi?

Unless tupate maelezo kuwa kuna mazungumzo ya siri ya kuwapatanisha na mwenye makosa amefahamika na ameomba msamaha kilichofanyika ni kizungumkuti tu na kuuziana mbuzi kwenye gunia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni