burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Ago 2017

JUX AFUNGUKA KUHUSU NGOMA YA ‘UTANIUA’ KUYAZUNGUMZIA MAHUSIANO YAKE NA VANESSA MDEE

Image result for JUX
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania Juma Mussa Mkambala a.k.a Jux ameyazungumzia mahusiano yake na muimbaji Vanessa Mdee na kwa namna ambayo wimbo wake mpya wa ‘Utaniua’ katika wazo la mahusinao  yake na kupatikana kwa wazo zima la wimbo.

Akizungumza na G.LOVETZ Jux amesema kuwa ingawa maandalizi ya kufanya wimbo huo kupitia mdundo uliotumika katika wimbo yalikuwepo lakini kukamilika kwa wazo la wimbo umezungumzia zaidi hali ya kimapenzi na kuachana kwake na mpenzi wake wa zamani muimbaji Vanessa Mdee.

“Sasa hivi ni miezi mitano tangu tume-break up, …kitu ambacho nimekiimba kwenye ile nyimbo ni kitu ambacho nilikuwa katika ile hali ya hivyo, kitu ambacho nimekiongea nimekitoa moyoni kwangu yaani ni nyimbo ambayo nimeiimba kutoka moyoni na mtu aliyesababisha kuimba kwenye ile nyimbo ni Vanessa” Amesema Jux.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni