burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

24 Ago 2017

Nay wa Mitego atoa ushauri kwa Diamond, Ommy Dimpoz na Alikiba


Nani kama mama? Rapper Nay wa Mitego ameonekana kuumizwa na silaha ya maneno mazito aliyoyatumia Ommy Dimpoz katika kumuangamiza adui yake.

Kupitia mtandao wa Instagram, Nay ameamua kuingilia kati kwa kuwataka wasanii hao Diamond, Ommy Dimpoz na Alikiba ambao kwa sasa vita yao inaonekana kuanza kufika mbali, wasiwaingize wazazi katika ugomvi wao huo.

Gombaneni, Loganeni Mpaka Muuwane… Napenda Kusikia Challenge Kwenye Game, Ila Tusiwaingize Wazazi Wetu🙏🏿 Please. Tutukananeni Matusi Yote Wenyewe Kwa Wenyewe Ikibidi Piganeni Kabisaaaa Atakae Kufa Tutazika na Itakua Historia Kama Big na Pac. Ila Kuwaingiza Wazazi ni U #Maku
Sipo Upande Wowote, Si #Kiba #Mond Wala #Ommy. Endeleeni na Vita yenu Kama Wanawake Mmechukuliana Mabwana. Ila Swala la Wazazi Mnavuka Mipaka #Maku nyie.!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni