burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

16 Sep 2016

Ben Pol: Nipo busy na show hadi December

14310754_1097548297007298_560585754_n
Moyo Mashine umekuwa na mafanikio makubwa kwa Ben Pol. Yeye pia amewahi kukiri hilo, na ndio maana anasema walau kila wikiendi kuanzia mwezi huu hadi December, yuko ‘booked’ kwaajili ya show
“Nina shows mpaka mwezi wa 12 tarehe 10 ndio show ya mwisho karibia wikiendi zote,” Ben alimuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
Amedai kuwa na ratiba hiyo ngumu kumemfanya akose muda mwingi wa kuingia studio kurekodi. Hata hivyo amedai kuwa ana collabo na msanii wa Nigeria, Chidinma, nyingine na msanii wa Ghana, Mr Eazy pamoja na ile aliyofanya na wasanii wa wa Afrika Kusini.
Kwakuwa Ben Pol anaamini kuwa Moyo Mashine inafanya vizuri bado, amedai hafikirii kuachia wimbo mpya hivi karibuni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni