burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

20 Sep 2016

DIAMOND PLATNUMZ AWAPA NENO MOJA AKISEMA WENYE WIVU WAJINGE

 Kanichambua kama karanga mama. Chambua kama karangaaa
Good morning mabibi na mabwana. Inatia moyo sana kuona msanii kutoka bongo land anaweka rekodi na kuivunja mwenyewe. Mpaka sasa hakuna msanii yeyote barani afrika ambaye Video zake zinatizamwa na watu wengi ndani ya muda mfupi kama Mondi Platnumz.
Sio kuwa tunajivunia Viewers ila tunajivunia Mziki wetu kutoboa zaidi Anga za kimataifa. 
Japo kuna watu wachache walioanza kuleta chokochoko na kutaka wimbo huu mpya ufungiwe kwa madai ya kutokuwa na maadili ila wengi wetu tunampongeza kwa ubunifu na kumsaidia Bi Saida karoli kurudi tena masikioni mwa watu. Binafsi baada ya kusikia wimbo huu niliamua Kudownload na wimbo wa Saida karoli ili nione kama ameutendea haki wimbo huo. 
Hongera Diamond platnumz na tunatarajia leo Tutahit 1M viewers ikiwa ni siku ya pili baada ya Salome Kufufuliwa.
Ujumbe wa leo " WENYE WIVU WAJINYONGE"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni