burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

16 Sep 2016

Billnas kujiunga na label mpya kubwa

Msanii wa muziki wa Hip Hop anayefanya vizuri na wimbo ‘Chafu Pozi’ Billnas amesema yupo kwenye mazungumzo ya kuhamia katika label kubwa ya muziki hapa nchini hivi karibuni.
Billnass
Rapper huyo ambaye kwa sasa yupo chini ya label yake ya ‘LFLG’, ameiambia glovetz kuwa kuna label nyingi zinamtaka kufanya naye kazi.
“Kusema kweli kuna mambo makubwa yanakuja, huwenda kazi yangu mpya ikaja nikiwa ndani ya label mpya,” alisema Billnas. Kuna label nyingi zimekuja na bado nipo kwenye mazungumzo, nadhani muda ukifika mtasikia tu,”
Billnas alianza kufanya vizuri na wimbo ‘Ligi Ndogo’ akiwa Rada Entertainment lakini baadae alihama katika label hiyo na kuanzisha label ya ‘LFLG’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni