burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

24 Sep 2016

GK adai Dogo Janja ndiye msanii wake bora kwa sasa ‘lazima nifanye naye ngoma’

dogo-janja

Msanii mkongwe aliyewai kufanya vizuri na Kundi la East Coast Team, King Crazy GK amefunguka kwa kusema kuwa rapa Dogo Janja ndiye msanii wake bora kwa sasa.

GK amesema anafurahishwa na jinsi rapa huyo anavyoweza kurap akiwa amerelax tofauti na wasanii wengine.
“Dogo Janja noma sana yule mtoto, nyimbo yake mpya inaitwa ‘Kidebe’, Dogo Janja ni rapa, angalia kwenye Kidebe alichokipanya, anarap yupo flexible. Yaani ana classics music,”  alisema GK
Aliongeza, “Muziki ni kama ukishajua kuogolea unaweza ukapiga mbizi, unaweza kufanya chochote unachotaka, mimi amenivutia sana nitafanya naye kazi moja,”
GK kwa sasa anafanya vizuri na video yake mpya ya wimbo ‘Nzuri Pesa’ ambayo achia wiki mbili zilizopita.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni