burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

24 Sep 2016

Ruby asema wimbo ‘Wale Wale’ sio dongo kwa mtu yeyote

ruby
Mwimbaji huyo ambaye ana sauti ya kipekee, ameiambia G.LOVE TZ kuwa wimbo ‘Wale Wale’ una ujumbe ambao utawafanya watu kujitambua na kujiondoa katika vifungo vya shetani.
“Mimi sijaimba huu nyimbo kwa ajili ya mtu yeyote kama ambavyo watu wanaweza kufikiria,” alisema Ruby. “Hii ni inspirational song, sijaimba mapenzi kabisa humo ndani kama ambavyo watu wanavyomuongelea Ruby anaimba mapenzi tu. Halafu sijamwongelea mtu nimemwongelea shetani, sifa za shetani,”
“Shetani siyo mtu wala hajafanana na mtu ila ni roho ambayo inaweza ikamwingia mtu yeyote. Hiyo roho inaweza ikaplay part mbili tofauti, hiyo roho inaweza ikakuletea kitu kizuri kumbe inataka ikitawale halafu ikuharibie, lakini kitu kizuri na chakudumu nichamungu. Na hivyo hivyo hivi vitu vinatokeaga kwa mabosi wetu, pengine bosi akakutaka kimapenzi ili akupandishe cheo, lakini ile hali siyo hali nzuri, kwa hiyo mimi sijamwongelea mtu yeyote bali ni shetani ambaye mara nyingi anataka kutuaribia maisha yetu,” aliongeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni