burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Feb 2017

Claudio Ranieri asema alikuwa ana ndoto ya kuendelea kuifundisha klabu ya Leicester City


Aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Leicester City Claudio Ranieri baada ya kufungishiwa virago wiki hii, amesema kuwa ndoto yake imepotea ya kuendelea kuifundisha klabu hiyo.
Ranieri mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza Leicester kushinda taji hilo licha ya kuorodheshwa kuwa na nafasi moja kati ya 5000 kushinda taji hilo.

Leicester sasa iko pointi moja juu ya eneo la kushushwa daraja huku ikiwa imesalia mechi 13.

“Baada ya furaha ya mwaka uliopita na kushinda taji la ligi nilikuwa na ndoto ya kusalia na Leicester. Kwa bahati mbaya haikuwezekana. Fursa hiyo ilikuwa nzuri na itakuwa nami maishani,” alisema Ranieri

Aliongeza, “Ninamshukuru kila mtu katika klabu hiyo,kila mtu aliyeshiriki katika ufanisi ,hususan mashabiki. Muliniweka katika nafsi zenu kuanzia siku ya kwanza na kunipenda.Ninawapenda nyie pia nami. Hakuna mtu anayeweza kuchukua kile tulichofanikiwa kupata pamoja na natumai munalifikiria hilo na kutabasamu kila siku ninavyotabasamu,”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni