burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Feb 2017

Steve Nyerere aikubali audio iliyosambaa mtandaoni, ni ile anayowazungumzia viongozi kuhusu sakata la Wema

Msanii wa filamu nchini na mchekeshaji Steve Nyerere amefunguka na kuizungumzia audio yake na Mama Wema Sepetu ambayo ilisambaa mtandaoni kuhusu sakata la Wema Sepetu na dawa za kulevya.
Aidha muigizaji huyo amedai hakuna msanii hata mmoja ambaye anakidai Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema mambo ambayo anasema Weme Sepetu kuwa anakidai chama hicho ni uongo na uzushi mtupu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumamosi hii baada ya kada mwenzake, Wema Sepetu kuhamia CHADEMA siku ya jana, Steve amedai Wema Sepetu ndiye msanii aliyelipwa pesa nyingi wakati wa kampeni za CCM 2015.

“Kati ya wasanii waliolipwa fedha nyingi na CCM ni dada (Wema Sepetu), na hakuna msanii wa Mama Ongea na Mwanao anayeidai CCM-Steve Nyerere. CCM tulifanya kampeni na tulilipwa, hatukuingia mkataba kuwa baada ya kampeni ukikamatwa na unga, CCM itakulinda na kukutetea,” alisema Steve Nyerere.

Kuhusu audio ambayo ilisambaa mtandaoni akizungumza na Mama Wema kusuhu sakata la Wema na madawa ya kulevya na kuwahusisha baadhi wa viongozi wa serikali na wabunge, Steve amedai siyo kweli kwamba alizungumza na viongozi hao kama alisema kwenye audio kwani alikuwa kumlaghai mama Wema Sepetu ili kumtuliza.

“Si kweli kuwa nilishinikiza wabunge wamjadili Wema, nilitumia sanaa tu kumlaghai Mama Wema atulie kuhusu Wema kukamatwa. Si kweli kuwa nilishinikiza wabunge wamjadili Wema, nilitumia sanaa tu kumlaghai Mama Wema atulie kuhusu Wema kukamatwa,” alisema

Aliongeza, “Sijazungumza na Waziri yeyote kuhusu Wema kukamatwa, nilitaka kumtuliza Mama. Ni kama kumlaghai mtoto na pipi achomwe sindano. Niwaombe radhi wote niliowataja katika mazungumzo yangu, sikufanya kwa nia mbaya, nilitaka kukilinda chama na kumsaidia Wema. Niliombe radhi Bunge tukufu, nimuombe radhi Spika Ndugai kwa kudanganya kuwa nilishinikiza Wabunge wamjadili Wema Sepetu. Nimuombe radhi Rais Magufuli kwa kuwatumia Mawaziri wake aliowaamini katika hili, lakini sikufanya kwa nia mbaya,”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni