burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

11 Feb 2017

Ningekuwa bado natumia Madawa ya kulevya jina langu lingetajwa na Makonda – Q Chief

Msanii wa muziki Q Chief amedai kuwa jina lake halikutajwa katika list ya RC Makonda kwa kuwa yeye tayari alishaachana na matumizi ya Madawa ya kulevya.

Muimbaji huyo amedai kutembea au kukaa na watu ambao wanatumia Madawa ya kulevya haimaanishi kwamba na yeye bado anaendelea kutumia.

“Mimi siko kwenye hiyo list na nilishaacha hizo mambo,” Q Chief alikiambia kipindi NLF cha EATV. “Ningekuwa natumia ungekuta jina langu kwenye list ya Makonda lakini mimi siko,”

Aliongeza, “Mimi ni mtoto wa uswahilini, nimekuwa huko kwa hiyo kutembea au kuonekana maeneo ambayo wanakaa wahumi ni maeneo yangu kwa sababu ndiko waliko washkaji zangu,”

Q Chief alidai yeye aliweza kuacha mwenyewe matumizi ya Madawa ya kulevya baaada ya kuona yanampotezea mwelekeo katika maisha yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni