burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Feb 2017

Kama mtu ananidharau kusaini WCB, hajui biashara yangu – Rich Mavoko


Muimbaji wa Kokoro, Rich Mavoko amedai kuwa kama bado kuna watu wanaona uamuzi wake wa kusainishwa na label ya Diamond, WCB ni kujishusha sababu yeye ni msanii mkubwa, hawaijui biashara yake.

“Mimi nakutana vitu vingi, mtu mwingine nyuma ya pazia haoni,” muimbaji huyo alikiambia kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir.

“Tunashoot, tunatoa video, tunarelease ngoma inahit, mimi ndo nakuwa napata tabu.Mtu anayesema nimejishusha kimuziki kujiunga WCB anakuwa hajui biashara yangu,” aliongeza.

Rich alisainishwa na WCB mwaka jana na kuachia wimbo wake wa kwanza, Ibaki Story.

Kwa upande mwingine, Rich alidai kuwa asipofanya muziki atakuwa akiwaandikia watu wengine mashairi na kwamba Tanzania ina upungufu mkubwa wa waandishi wa Bongo Flava.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni