burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

11 Feb 2017

Mtoto wangu wa pili nilizaa na Solo Thang – Wastara

Image result for wastara
Kumbe staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, aliye mama wa watoto watatu, mmoja kati yao, alizaa na mkongwe katika Bongo Hip Hop, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’.

Akiongea wiki hii katika kipindi cha Uhondo cha EFM, Wastara alisema mtoto wao huyo kwa sasa ana umri wa miaka 13.

“Mtoto wangu wa pili kwa sasa ana miaka 13, nimezaa na Msafiri Kondo (Solo Thang),” alisema muigizaji huyo ambaye pia ni mfanyabiashara.

Kwa sasa muigizaji huyo anatoka kimapenzi na msanii wa filamu Bondi Bin Sinani ambaye pia  ni meneja anayesimamia kazi zake za filamu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni