burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

18 Feb 2017

Rapper AKA na mtangazaji Bonang Matheba wamwagana


Rapper AKA ametangaza kupitia Twitter kuwa yeye na mtangazaji wa redio na TV, Bonang Matheba wameachana.

Wawili hao walirejea kutoka kwenye mapumziko nchini Thailand wiki chache zilizopita na siku moja tu iliyopita walikuwa wakioneshana mahaba kwenye mitandao ya kijamii.

“Sad to announce that myself and Bonang have broken up. We tried guys,” alitweet AKA.

Hii ni mara ya pili AKA anatweet kuhusu kuachana na Bonang. Mwaka jana alisema hivyo pia lakini aliifuta post dakika chache baadaye, akisema kuwa waligombana na kisha kuachana.

Bonang bado hajazungumza chochote kuhusu kuachana kwao. Katika msimu wa sikukuu mwishoni mwa mwaka jana, AKA alimkunisha Bonang na ndugu zake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni