burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Feb 2017

Hii ndio ratiba ya michuano ya kombe la Europa


Ratiba ya michuano ya kombe la Uefa Ueropa League katika hatua ya robo fainali imetoka huku michezo ya awali ikitarajiwa kuchezwa Machi 9 na marudiano ikiwa ni Machi 16.

Mechi zinazosubiriwa kwa hamu kubwa ni pamoja na Olympique Lyon ya Ufaransa iliyopangiwa kucheza na AS Roma ya Italia na mechi nyingine ikiwa ni Schalke 04 dhidi ya Borussia Monchengladbach (zote zinacheza ligi kuu ya Ujerumani).

Kutokana na kiwango kwa sasa kutoka kwa Manchester United inapewa asilimia kubwa ya kuingia katika hatua ya nusu fainali ya kombe hilo kutokana na kupangiwa timu ya Rostov kutoka Urusi ambayo inashika nafasi ya saba katika ligi ya kwao.

Wakati huo huo timu ya Mbwana Samatta KRC Genk imepangiwa kucheza na KAA Gent (zote kutoka Ubelgiji) ambayo iliitoa Tottenham Hospurs katika hatua ya timu 32 bora.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni