burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

3 Feb 2017

Ditto: Jina langu lilitajwa kimakosa kwenye orodha ya wanaotumia unga


Jina la Ditto liliibua minong’ono kwa watu wengi pale mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipolitaja kwenye orodha ya wasanii wanaotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya.

Akili ya watu wengi moja kwa moja ikaelekea kwa hitmaker wa ‘Moyo Sukuma Damu’, Lameck Ditto. Muimbaji huyo kupitia mtandao wa Instagram amewatoa hofu mashabiki wake kwa kukanusha kuhusika katika orodha hiyo na kudai kuwa jina lake lilitajwa kwa makosa.

Kupitia mtandao huo, Ditto ameandika:

Kwenye ile Clip maarufu inayosambaa, jina langu lilitajwa kwa bahati mbaya. Kulitokea makosa kwenye matamshi na walirekebisha pale pale, Binafsi sijawahi kujihusisha na hayo mavitu yanayotajwa hata siku moja. Na kwa wanaonijua vizuri wanafahamu vyema kuhusu hilo. Kwa hiyo natumia nafasi hii kuwasihi walioona Clip hiyo na kuwapa wasiwasi kuhusu mimi ondoeni wasiwasi huo. Mimi siyo mmoja wao na kwa kudra za Mungu sitakuwa hivyo hata siku moja

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni