burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

11 Feb 2017

Young Dee avamiwa na kuibiwa simu na pochi, amtuhumu Van Dame


Msanii wa muziki wa hip hop, Young Dee amefunguka kwa kudai kuwa usiku ya juzi alivamiwa na mtu anayedaiwa kuwa ni Van Damme wa Sinza ‘Damme’ na kuporwa simu pamoja na pochi yake ambayo ndani ilikuwa na vitambulisho mbalimbali.

Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Young Daddy’ ameomba kwa yeyote atakaye okota kitambulisho chake atoe taarifa.

Usiku Wa kuamkia juzi, tulivamiwa na jamaa anaesemekana ni Dame Wa sinza, nikiwa nimekesha studio maeneo ya sinza palestina kwa Mr T Touch,” aliandika Young Dee Instagram.

Aliongeza, “Sasa juhudi za kumpata zimekua ngumu maana amekua na matukio ya hivo mara kwa mara juzi kaiba simu mbili moja ni yangu (iphone6s+) na Samsung na wallet yangu iliyokua na vitambulisho vyangu pamoja na Card ya bank, Sasa kwa yoyote ataepata taharifa itayoweza kunisaidia naomba anifate Dm tafadhari! 🙏 Tag wana wote Wa sinza tusaidiane kwa hili!,”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni