burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

19 Nov 2016

Barnaba afunguka faida aliyoipata baada ya kuachia ‘Lover Boy’

Msanii na mtayarishaji wa muziki Barnaba ametaja faida aliyoipata baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Lover Boy’.
15043882_695331390634946_6717057194262528000_n
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Storm cha Clouds TV kuwa wimbo huo umekuwa ya kwanza kumpatia show nyingi kwa muda mfupi na dili nyingine za matangazo.
“’Lover Boy’ ni wimbo ambao umenifanya nipate show nyingi kwa muda mfupi zaidi pamoja na kupata dili kibao za matangazo ya makampuni mbalimbali pamoja na endossement nyingine nyingi,” amesema Barnaba.
‘Lover Boy’ ni moja kati ya nyimbo kali usiyochoka kuisikiliza huku ikiwa imeshatazamwa zaidi ya mara laki 5 kwenye mtandao wa Youtube tangu ilipotoka mwezi Septemba mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni