burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

26 Nov 2016

Siku Lady Jaydee akitupa order tucheze nyimbo zake tutaanza kucheza – Ruge (Audio)

Ruge Mutahaba amesema siku Lady Jaydee akiwaambia waanze kucheza nyimbo zake watafanya hivyo.
Bosi huyo wa Clouds Media Group, ametoa kauli hiyo Ijumaa hii kwenye mahojiano na kipindi cha XXL cha kituo hicho. “Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema.
Ruge amesema ana muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo amedai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’
Wiki kadhaa zilizopita Ruge na Joseph Kusaga walishinda kesi ya kuchafuliwa (defamation) iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Lady Jaydee na muimbaji huyo kuamriwa kuwaomba radhi.
“Tunashukuru walau tulishinda ile kesi lakini at least ilitengeneza mfano wa watu kuelewa kwamba tusipende kutuhumu vitu kama watu huna uhakika. Bahati nzuri pia hata katika hiyo kesi alisema mwenyewe hajawahi kusikia tunasema, aliambiwa na watu. Lakini ni mambo yashapita hayo.”
Mtazame hapo chini Ruge akizungumzia bifu ya Diamond na Alikiba, Clouds na yeye kulaumiwa, tofauti yake na Ruby pamoja na lawama za hivi karibuni za TID.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni