burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

29 Nov 2016

Fid Q na Joh Makini waeleza kwanini hawajafanya collabo hadi sasa (Audio)

Kama wewe ni shabiki wa hip hop, bila shaka utakuwa na hamu ya siku moja kuwasikia Joh Makini na Fid Q kwenye ngoma moja. Kwanini hadi sasa hawajafanya wimbo pamoja?
fid-22
Mtangazaji wa Jembe FM, JJ alizungumza na rapper hao waliokuwa pamoja jijini Mwanza kuhusiana suala hilo.
“Collabo hiyo bado haijashindikana nadhani bado haijafikiriwa tu lakini muda wake ukifika itafanyika,” alisema Fid.
Kuhusu anavyowachukulia Weusi, Fid alisema, “Wanafanya kile kitu wanachokiamini na kinawalipa na hiyo ndio sanaa yenyewe, fanya kitu ambacho unaamini. Usifanye kwasababu mtu fulani anafanya au mtu fulani kakuambia fanya,” aliongeza Fareed.
Kwa upande wake Joh Makini alisema, “mimi nafikiri ni time tu, muda ndio unasema wakati mwingine. Sababu hatujawahi kuwa na tatizo naye, watu wengine wanachukulia hivyo. Mimi nafikiriaga ni kama ushindani tu wa kwenye muziki ambao lazima uwepo ili kuongeza utamu. Lakini no hard feeling, anytime pengine.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni