burudan

https://share.bannersnack.com/bdtkqutzy/

29 Sep 2016

Msanii Chidy Stress akana mimba ya mtoto wa kigogo akidai hamjui


Msanii ambae anafanya vizuri na wimbo wake wa ongeza kidogo anaefahamika kwa jina chidy stress hivi juzi kati alionekana kuwa skendo inayomuhusisha mtoto wa kigogo



chidy stress akiongea na g.lovetz alisema kuwa hizi habari sio za kweli na hazina hata chembe ya ukweli ni watu tu wanazusha 


stress aliongezea kuwa kitu anachofanya anajua na yuko makini sana kwa mambo yake ingawa kuna watu wanamzushia tu stori za ajabu ajabu pia ninawaomba mafansi wanaopenda mziki wangu nawapenda sana mana bila wao hakuna mziki tena alimaliza chidy stress

Stamina kuachia albamu mpya Disemba, itakuwa na nyimbo 15

Stamina2

Rapper Stamina baada ya kufanya vizuri na albamu yake ya ‘Mt Uluguru’ anajipanga kuachia albamu mpya mwezi Disemba ambayo itakuwa na nyimbo 15

Akiongea na glovetz wiki hii, Stamina amesema tayari ameshamaliza kurekodi nyimbo zote za albamu hiyo na sasa ipo katika hatua za mwisho za maandalizi ya kutoka.
“Albamu mpya kwa sasa ipo jikoni kwa Rash Don, nimeshamaliza kurekodi na Disemba inaingia sokoni,” alisema Stamina. Nashukuru mungu hii ni tofauti ili iliyopita, mapaka sasa ninapozungumza na wewe tayari kuna wadhamini wamejitokeza kwa ajili ya usambazaji pamoja na kuandaa matamasha ya uzinduzi,”
Rapper huyo amesema nyimbo hizo 15 amefanya na maproducer tofauti tofauti ili kupata ladha tofauti katika kila wimbo.
Albamu iliyopita ya ‘Mt Uluguru’ iliuza nakala 9,000.













New Audio I Ramso-boy-VIJISABABU I DOWNLOAD

Diva: Mastaa wa Bongo waelewe thamani yao, mimi nachaji milioni 3.5 kwa appearance tu

14499008_1178700912227015_8539192551284932608_n

Mtangazaji wa Clouds FM, Diva The Bawse amewataka mastaa wa Tanzania kutambua thamani ya brand zao na kuacha kujichukulia poa.

Amedai kuwa mastaa wengi wamekuwa wakitumika bure kufaidisha watu wengine na anadhani ni muhimu wakaacha kujishusha kiasi hicho.
Anadai kwa upande wake yeye, hafanyi kitu bure na kudai kuwa hata kuonekana kwenye saa moja kwenye party ya mtu, ni lazima awe amemlipa.
“My standard rate is 3.5 million in one night that including 30 minutes hosting, na sikai less than hour naondoka,” Diva ameandika kwenye blog yake.
“Ifike stage celebs wajue value yao na sio kutumika tu kwa faida ya watu wengine. Chochote unaona pia napost kwenye account zangu za mitandao kinalipiwa., lazima ujue kama wewe ni maarufu lazima ulipwe hata kutweet brand ya mtu mwingine,” ameongeza.
Mtangazaji huyo ana zaidi ya followers milioni 1.1 kwenye Instagram na amekuwa akiingiza mkwanja mrefu kwa kupost matangazo mbalimbali.



Nuh Mziwanda azinguana na uongozi wake, adai viongozi wanataka umaarufu kuliko kazi

nuh

Mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amezinguana na uongozi wake ambao alikuwa anafanya nao kazi kwa madai umeshindwa kufanya kazi aliyoitaka.

Mapema mwaka huu Petit Man alimchukua msanii huyo na kuamua kumsimamia ikiwa ni wiki chache toka aachane na wasanii wa Endless Fame ya Wema Sepetu.
Nuh amedai yeye ni msanii mkubwa na meneja huyo ameshindwa kumfikisha pale ambapo alikuwa anataka kwenda.
“Nimetoka kule kwa ajili tu ya sababu zangu binafsi inabidi ni’move on, mi sio msanii mdogo inabidi niwe na meneja ambaye anajielewa na anajua msanii ambaye ninaye ni msanii ambaye yupo katika level gani, kama meneja anashindwa kujua msanii ambaye anafanya naye kazi siwezi kudeal naye, kwa sababu nilishapotezaga time katika muziki three years kwenye mapenzi, sa siwezi kupoteza mwezi mmoja kwa mtu ambaye kanikuta tu nimeamua kufanya naye kazi, kwa hiyo ni bullshit mi naachana naye naendelea na mambo yangu mengine”, Nuh Mziwanda alikiambia kipindi cha Planet bongo cha EA Radio.
Aliongeza, “Siyo kwa ubaya kwa uzuri, niliamua kufanya naye kazi, lakini kashindwa kupresent kile kitu ambacho mi nilikihitaji, narudia tena mi ni msanii mkubwa, inabidi ajue msanii mkubwa inabidi awe na nini na nini, kuna vitu avijue kama meneja, sasa kufanya kazi na meneja ambaye na yeye anataka ustar, ni kitu ambacho hakiwezekani”, alisema Nuh Mziwanda.
Nuh Mziwanda pia alisema anaamini jitihada zake ndizo zimemfikisha hapo alipo, na kukanusha kauli ambayo watu wengi wamesema kuwa kwa kuwa sasa ana studio, amekuwa na dharau kwa uongozi wake.





Young Killer aamua kubadilika ‘ngoma yangu mpya inayokuja ni best kuliko…’

young-killer

Mkali wa kuchana, rapa Young Killer Msodoki amesema ameamua kuwafurahisha mashabiki wa muziki wake kwa kufanya baadhi ya mabadiliko katika nyimbo zake.

Akiongea na glovetz  wiki hii, rapa huyo amesema wimbo wake mpya ambao atauchia hivi karibuni utakuwa ni moja kati ya nyimbo zake bora.
“Labda niwaambie kitu kimoja hii ni exclusive, ngoma yangu ambayo nitakuja kuitoa baada ya hii ‘Mtafutaji’ ndo ngoma yangu best kabisa,” alisema Young Killer.
Aliongeza,”Sio best kuliko zote zilizopita, lakini hii inayokuja ni best kwa sababu ni ngoma kali kiukwei yaani naamini watu watapenda kiukweli. kwa hiyo ubora wake nazungumzia utunzi, jinsi ambavyo style imeifanya, uandishi nimebadilisha, kuna vitu vimekuwa imara zaidi, kwa hiyo mimi nasema mashabiki wangu wakae mkao wa kula,”
Rapa huyo amesema kabla ya kuachia wimbo huo ataachia kwanza video ya wimbo ‘Mtafutaji’ ambao aliuachia wiki chache zilizopita.








Mwana FA awataja rappers wawili wa sasa Bongo anaowakubali zaidi

14374474_1615930842032624_4195279520216907776_n

Mwana FA amewataja Bill Nas na Darassa, kuwa ndio rapper wa kizazi cha sasa anaowakubali zaidi.

Amewataja Jumatano hii wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Campus Vibes cha Times FM.
“Bill Nas, Bill Nenga yupo hapo yaani without a doubt hata ukiniamsha saa nane usiku,” alisema Mwana FA. “Amepatia, muziki wake anavyotaka uwe ndio umekuja hivyo na wananchi wamemuelewa.”
FA anasema yeye ndiye aliyeanza kumtambulisha Nas kwa watu wa habari na anafurahi kuona kuwa amefahamika tayari na watu wanakubali muziki wake.
“Kafanya juhudi nyingi sana, namjua,” alisisitiza FA.
Pia rapper huyo mkongwe anaamini Darassa ni rapper wa moto ambaye huu ni wakati wake. “Darassa yuko vizuri sana nafikiri na yeye kahangaika sana na ameupatia sasa hivi.”
Kwa upande mwingine FA aliwataja rappers watano anaowakubali zaidi kwa muda kuwa ni Hashim Dogo, Profesa Jay, Fid Q, Jay Moe na Solo Thang.


28 Sep 2016

Ray C afunguka barua kuwapongeza Diamond na Zari

14515741_580289242159270_1348646149287837696_n

Ray C amefunguka kwa mara ya kwanza na kutoa kauli yake juu ya couple ya Diamond Platnumz na Zari The Bosslady.

Kupitia mtandao wa Instagram, malkia huyo wa kiuno bila mfupa amedai kuwa uchapakazi wa wawili hao ndio umempelekea azidi kuwapenda.
Seriously Namaste lil bhaia!ngoja niwe mkweli wa nafsi yangu nipate nafuu dude!that Salome of Yours is damn hot!The Powerful couple in this industry kwa sasa bila ubishi wangu ni hawa wachapakazi wawili,bidii katika kila walifanyalo,go getters,wanavyopeana nguvu katika kazi zao,team work team work team makes everything go the it should be and that makes me fall in love with these two hard working souls!everysecond of the day,lil bro u really smart dude,i respect you for that roho ya upendo ulionayo ndio inayozaa matunda bora ya vipaji lukuki vinavyotamba sasa angalia Raymond!Harmonize!!!! Angalia upendo wako unavyozaa matunda bora,Mungu sio kipofu anaona lil bro!Baraka zake kwako hazitaisha dogo you deserve every penny lil bhaia! am a fan all the way keep chasing tht paper,i admire your management team,how serious you guys are in ths industry of ours..I don’t call u Simba no more dude! I call you THE GURU OF THE INDUSTRY!haaaaaaaaaa nilitaka kusahau mama weee baiiiiiiiii the wayyyyyyyyyyyyy kale kapicha kangu kalikobandikwa wasafi studios weeee eeeeee weeeee nimejishauaje sasa weweeeee mpaka mama angu nimemringishiaaaaaaaa kaka angu nimemringishiaaaaa mjomba nimemringishiaaaa yani acha weweeee nimefurahi saaaaana sana umenipa moyo mdogo wng ASANTE SAAAAANA ,Thats very kind of you lil bro!STAY BLESSED LIL BHAIA! @diamondplatnumz And I am Your Shabikj Makini without any reasonable doubt……….


Ben Pol: Msanii kujisimamia mwenyewe inaua ubunifu

alke9121

Ben Pol anaamini kuwa pindi msanii anapojisimamia mwenyewe, anapoteza ubunifu muhimu anaouhitaji ili kufanikiwa

Anadai kuwa ni muhimu kwa msanii kuwa na management au watu wa kumsaidia.













Salamu za Mrisho Mpoto kwa Diamond Platnumz kuhusu wimbo wa Salome

Moja kati ya wasanii wenye heshma kubwa nchini na watunzi wa mashairi na nyimbo zenye mahadhi ya kiafrika, Mrisho Mpoto, kupitia mtandao wa Instagram amemsifia Diamond Platnumz kwa wimbo wake mpya wa Salome na kusema kuwa amemfurahisha sana kwani amefanya wimbo wenye asili ya kwetu Tanzania na hiyo ni heshima kwa nchi.
 >>Nassibu kiukweli nimefurahishwa sana na kazi yako ya#Salome imeonyesha ukomavu Mkubwa na team work, kikubwa ukiwa unafanya kazi zenye test ya nyumbani unatupa heshima kama nchi na inakuonyesha wewe ni nani? na nani siyo wewe? Nassibu Mwenda kwao siku zote haogopi Giza, nenda lakini waambie nna kwetu, kama ulivyofanya kwenye Salome. Sisi ni wabantu bwana tunaruhusiwa zaidi ya mmoja, na Mimi ntamtafuta Salome wangu wa ukubwani ashike magoti nisimame kama ngongoti japo nna kitambi ntainama kidogo!!@diamondplatnumz @babutale
mpoto

Tuzo nyingine kubwa ambayo Alikiba amechaguliwa kuwania


Majina ya washiriki katika  tuzo kubwa mbalimbali yamekua yakiendelea kutajwa na tuzo nyingine ambayo majina ya wanaowania  yametajwa ni tuzo za MTVEMA, ambazo Alikiba ametajwa kuwania kama msanii bora kutoka Afrika.
Tuzo za ( MTVEMA ) MTV Europe Music Awards  ni tuzo za mziki za MTV barani Ulaya ,kama ilivyo MTVMAMA kwa Africa.  Kupitia mtandao wake wa Instagram Alikibaameeleza jinsi ambavyo mashabiki wake wanaweza kumpigia kura.
kiba

Dully Sykes awataja wasanii watatu aliowasaidia na leo wanalipa fadhila

Msanii mkongwe katika muziki wa Bongo Flava, Dully Skyes amesema katika wasanii wote ambao aliwahi kuwasaidia kimuziki mpaka wakafanikiwa, ni watatu tu ndio ambao wamekuwa wakilipa fadhila kwake na ambao wamekuwa wakimpigania.
dully_2_0
Dully Skyes alisema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo na kudai amewasaidia wasanii wengi lakini wengi wao wanaishia kumuita tu ‘brother’ lakini si Diamond Platnumz, Mr Blue na Queen Darlin.
“Watu ambao nimewasaidia wananipa heshima ni wawili tu, wengine wanaishia kuniita brother D tu, lakini Diamond Platnumz, Mr Blue pamoja na Queen Darlin ndiyo wananipa ile heshima kabisa na wana uchungu na mimi kwamba huyu kaka yetu. Kwahiyo katika wale watoto ambao nimewatoa kwenye muziki wakiwa wadogo na wananisaidia ni hao watatu,” alisema.
Hivi karibuni Diamond kupitia label ya WCB alimpa ofa Dully ya kughramia mradi mzima wa wimbo wake unaoendelea kufanya vizuri, Inde akiwa na Harmonize.

Jokate aja na mkakati wa kuwakomboa wasusi wa nywele

Ususi ni miongoni mwa ajira iliyoajiri maelfu ya akinamama nchini huku wengi wakiendesha familia zao na kusomesha watoto wao kwa kazi hiyo. Lakini fani hiyo haijawahi kurasimishwa ipasavyo licha ya kuwa kimbilio la wanawake wengi wanaopenda kupendeza.
14448420_191801451251021_548995905324318720_n
Kwa kulitambua hilo, Jokate Mwegelo kupitia brand yake ya Kidoti, akishirikiana na kipindui cha Leo Tena cha Clouds FM, wamekuja na kampeni iitwayo Msusi Wao yenye lengo ya kuwawezesha kiuchumi wasusi nchini.
14360095_172467366530022_6060166603746574336_n
Jokate akiwa na wadhamini na washiriki wa kampeni hiyo wakati wa kuitambulisha Jumanne hii
“Kiukweli wasusi walioweza kufika licha ya muda mdogo mmenipa moyo. Sasa basi siku zenu za kuchuliwa poa kama wasusi ziishe leo. Ujuzi wako huu ndio ajira yako ndio kitu kitakocholisha familia yako na kuiendeleza taifa letu. Tuipe thamani, tuwe wabunifu zaidi na kutengeneza fursa zaidi,” ameandika Jokate kwenye Instagram.
Chini ni picha zaidi za Jokate wakati wa kutambulishwa kwa kampeni hiyo.
14295524_549157495279064_6918041400059625472_n
Katika kampeni hiyo, Jokate ameazimia kuwasaidia wasusi ambao hawana saluni maalum za kufanyia kazi zao.
“Kila moja wetu ana wajibu wa kumuinua mwenzake kutokana na uwezo wake na kile kidogo alichojaaliwa,” anasema.
14359376_1112255425527790_7040648916630503424_n

Baby J alilia ushirikiano kwa wasanii wa kike

Baby J 1

Msanii wa muziki kutoka visiwani Zanzibar, Baby J amesema ushirikiano kati ya wasanii wa kike ndio kitu pekee ambacho kitawakomboa wasanii wengi wa kike na kufanya vizuri zaidi kitaifa na kimataifa.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya kazi chini ya Mkubwa Fella, ameiambia glovetz  kuwa wasanii wengi ambao wanafanya vizuri wanawavimbia wenzao hali ambayo amedai inapoteza ushirikiano.

“To be honest wasanii wa kike hatuna ushirikiano, wasanii wakike hatupendani hasa hawa ambao wanafanya vizuri au umeshapata nafasi,” alisema Baby J. “Wenzetu wakiume wanashirikiana hata japo kwa uongo lakini tunaona wanashirikiana, lakini wasanii wa kike ushirikiano ni mdogo sana na kinachosababisha kuna ile chembe chembe ya ‘ujana jike’, yaani kuna yale mambo fulani wa kike ambao tunao,”
Muimbaji huyo amesema ushirikiano kati ya wasanii wa kike kunaweza kusaidia kuongeza idadi ya wasanii wa kike wataofanya vizuri kwenye muziki.

New Audio I Black wa Uswazi - MANENO I DOWNLOAD

New Audio I Sam wa Ukweli - KISIKI I DOWNLOAD

New AUDIO I Rich mavoko Ft Raymond - Merry me[Slow Version] I DOWNLOAD

New Audio I Aslay - Kidawa I DOWNLOAD


24 Sep 2016

Bushoke: Watu wengi wananiomba nifanye wimbo na Christian Bella

13628450_1022930347814908_1334417226_n

Hebu fikiria Dunia Njia na Usilie vikiunganishwa na kuwa wimbo mmoja itakuaje?

Au Bushoke na Christian Bella wakiingia studio kufanya wimbo wa pamoja! Hicho ni kitu ambacho mashabiki wengi wanakitamani.
Akiongea na mtangazaji wa ABM Radio ya Dodoma, Dj Rodger, Bushoke amesema amekuwa akiambiwa na watu wengi afanye wimbo na Bella na kwamba mpango huo upo.
Bushoke amedai kuwa mashabiki wanaamini kuwa collabo yake na Bella itakuwa tofauti na itafanya vizuri pia kajipanga na hii game ya sasa na kawaaomba mashabiki wake kuwa tayar kuipokea collabo hio matata soon itakuja 

New Audio I Tox Star Ft. Barnaba - Chillax I DOWNLOAD


Ruby asema wimbo ‘Wale Wale’ sio dongo kwa mtu yeyote

ruby
Mwimbaji huyo ambaye ana sauti ya kipekee, ameiambia G.LOVE TZ kuwa wimbo ‘Wale Wale’ una ujumbe ambao utawafanya watu kujitambua na kujiondoa katika vifungo vya shetani.
“Mimi sijaimba huu nyimbo kwa ajili ya mtu yeyote kama ambavyo watu wanaweza kufikiria,” alisema Ruby. “Hii ni inspirational song, sijaimba mapenzi kabisa humo ndani kama ambavyo watu wanavyomuongelea Ruby anaimba mapenzi tu. Halafu sijamwongelea mtu nimemwongelea shetani, sifa za shetani,”
“Shetani siyo mtu wala hajafanana na mtu ila ni roho ambayo inaweza ikamwingia mtu yeyote. Hiyo roho inaweza ikaplay part mbili tofauti, hiyo roho inaweza ikakuletea kitu kizuri kumbe inataka ikitawale halafu ikuharibie, lakini kitu kizuri na chakudumu nichamungu. Na hivyo hivyo hivi vitu vinatokeaga kwa mabosi wetu, pengine bosi akakutaka kimapenzi ili akupandishe cheo, lakini ile hali siyo hali nzuri, kwa hiyo mimi sijamwongelea mtu yeyote bali ni shetani ambaye mara nyingi anataka kutuaribia maisha yetu,” aliongeza.

Trey Songz amzunguzia Vanessa Mdee na jinsi alivyomkubali

ctfs1prwgaapu31
Wakati akijibu swali hilo muimbaji huyo wa Marekani amesema wametengeneza wimbo mzuri pamoja.
“Vanessa is great, we got a great song together, has a great chemistry, she loves to laugh and joke even when we was performing having a good time,” alisema.
Kuna uwezekano mkubwa Vanessa na Trey Songz wakaka kutengeneza wimbo wa pamoja nje ya Coke Studio.

GK adai Dogo Janja ndiye msanii wake bora kwa sasa ‘lazima nifanye naye ngoma’

dogo-janja

Msanii mkongwe aliyewai kufanya vizuri na Kundi la East Coast Team, King Crazy GK amefunguka kwa kusema kuwa rapa Dogo Janja ndiye msanii wake bora kwa sasa.

GK amesema anafurahishwa na jinsi rapa huyo anavyoweza kurap akiwa amerelax tofauti na wasanii wengine.
“Dogo Janja noma sana yule mtoto, nyimbo yake mpya inaitwa ‘Kidebe’, Dogo Janja ni rapa, angalia kwenye Kidebe alichokipanya, anarap yupo flexible. Yaani ana classics music,”  alisema GK
Aliongeza, “Muziki ni kama ukishajua kuogolea unaweza ukapiga mbizi, unaweza kufanya chochote unachotaka, mimi amenivutia sana nitafanya naye kazi moja,”
GK kwa sasa anafanya vizuri na video yake mpya ya wimbo ‘Nzuri Pesa’ ambayo achia wiki mbili zilizopita.


Dude kuileta Bongo Dar es Salaam October 2016

NI Sept 20, 2016 ambapo msanii kutoka Bongo Movie, Dude amefunguka kuhusu maandalizi ya kuirudisha kipindi cha Bongo Dar es Salaam katika luninga.
Akiongea G.LOVE TZ staa huyo alisema…>>>Kwanza nilikuwa najaribu kufanya mazungumzo na wamiliki wa vituo vya luninga ili niweze kurusha kipindi changu cha Bongo Dar es Salaam na sio kama nahitaji pesa nyingi sana lakini nahitaji aghalau nirudishe maandalizi ya kazi yangu’
‘Takribani tukiacha mwezi huu wa tisa upite tutegemee mwezi wa kumi nadhani kila kitu kitakuwa vizuri na nitaweza kutengeneza vipindi vingi zaidi na mwezi wa kumi nina uhakika kabisa kuwa kipindi kitakuwa hewani lakini sitotaka kuwaambia mashabiki zangu kuwa ni TV gani kitakuwa kinarusha ila wakae mkao wa kula’

Rekodi nyingine iliyovunjwa na Diamond Platinumz Youtube

Rekodi za mastaa wa muziki kutoka Afrika zinazidi kuwekwa na kuvunjwa kila siku kutokana na kazi nzuri wanazozitoa. Mtu wangu leo nimeipata rekodi hii aliyoivunja msanii Diamond Platinumz kutoka Tanzania baada ya kuachiwa tu kwa video yake ya Salome aliyomshirikisha msanii Rayvanny kutoka lebo yake ya Wasafi Classic  Baby (WCB).
salome
Najua inaweza kua sio jambo geni ukisikia wimbo wa msanii kutoka Marekani umetazamwa mara nyingi kupitia Youtube, Lakini leo hii niko na hii kutoka Tanzania mtu wangu, Diamond Platinumz amefanikiwa kuweka rekodi ya kufikisha Views zaidi ya Milioni moja na nusu kwenye mtandao wa Youtube baada ya Video ya hit single ya Salome kuwekwa ndani ya siku nne tu.
Diamond Platinumz anafuatana kwa views nyingi na wasanii mapacha kutoka kundi la PSquare na video yao ya Bank Alert iliyotazamwa zaidi ya mara milioni moja na laki moja ndani ya wiki moja tangu ilipowekwa Youtube.
salome
Video ya PSquare inasemekana kuwa imepata views nyingi kutokana na matatizo yaliyokuwepo kati yao na kupelekea kutangaza kuwa kundi limevunjika na sababu kuwa ikitajwa kuwa kaka yao mkubwa Judees Okoye ndiye alikua chanzo cha wao kutofautiana.
Ndani ya Bank Alert wanaonekana mastaa mbalimbali kama Onyeka Onwenu, Mr Ibu, Phyno na Kcee ambao pia wamechangia kuisogeza video hiyo mpaka hapo ilipo.

Nuh Mziwanda kaelezea sababu za kuachana na Meneja Petit Man

Ni September  22, 2016 kwenye U HEARD ya Clouds FM, inamuhusu Nuhu Mziwandaambaye amemlalamikia aliyekuwa Meneja wake, Petit Man, Nuhu Mziwanda amedai kuwa amekuwa akichukua pesa kwa kutumia jina la Mziwanda halafu hazifikishi kwake. Soudy Brown amepiga nao story leo kwenye U Heard huku Nuh akieleza sababu za kuamua kuachana na usimamizi wa Petiman.
>>>kama meneja ambaye anafanya kazi na wewe anashindwa kujua wewe ni mtu gani kwenye jamii huyo ni tatizo, mimi natafuta pesa kwa jina langu sasa yeye asitumie ile kusema mimi ni meneja wa nuh kupata pesa halafu hazifikishi kwangu hiyo ndo sababu mimi nimemkacha:- Nuh Mziwanda

Navy Kenzo waeleza furaha kutajwa kuwania MTV MAMA 2016

Sept 21, 2016 majina ya wasanii watakaowania tuzo za MTV MAMA 2016 yalitajwa huku Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz na kundi la Navy Kenzo pamoja  na Alikiba ndio wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania tuzo kubwa za Africa za MTV Africa Music Awards 2016.
Sasa G.LOVE TZ imewapata Navy Kenzo huku wakayaongea haya>>>Tunashukuru sana tumepata taarifa za MTV MAMA 2016 tumechaguliwa kwenye Best Group yaani tumefurahia sana ni kitu ambacho kimetutia nguvu sana
Kimeonesha jinsi gani kazi yetu ambayo tuliyokuwa tukifanya kwa muda mrefu ndio imeanza kuleta matunda hayo kwahiyo tunashukuru sana, tutatoa maelekezo katika mitandao yetu ili mashabiki wetu na wengineo wajue jinsi ya kutupigia kura’

Vanessa Mdee aeleza collabo yake na Trey Songz….

Ni Headlines za Vanessa Mdee ambae amekuwa ni moja kati ya wasanii wa Africa waliochaguliwa kurekodi wimbo na mshindi wa Grammy na mwimbaji wa RNB nchini Marekani, Trey Songz kupitia msimu wa 4 kipindi cha Coke Studio Africa.
 Vanessa Mdee aliyaongea haya>>>Niko Kenya nikifanya msimu wa Coke Studio Africa ambapo msimu huu tumemkaribisha msanii wa kimarekani Trey Songz kuja kufanya collaboration na waafrika nikiwemo na mimi’
‘Ni experience ya kipekee sana nimefuraha sana kuwa katika nafasi hii ya kufanya collabo nae kwani ni hatua nzuri kwangu pia kuitangaza nchini yangu’

Magic FM kuja na muonekano na vipindi vipya

dsc02400

Kituo cha redio cha Magic FM, kinachomilikwa na kampuni ya Afrika Media Group kinatarajia kuzindua muonekano mpya wa redio hiyo Septemba 26 mwaka huu samabamba na uboreshaji wa vipindi baada ya kutorusha matangazo yake takribani siku 26

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa vipindi, Orest Kawau, amesema muonekano wa kituo hicho umetokana na maoni ya wasikilizaji kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo masafa ya redio yanawafikia katika mkoa wa Mwanza, Dar es Salaam, Arusha, Morogoro pamoja na Tanga.
“Baada ya utafiti wetu kutoka kwa wadau wetu kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania, tumeboresha vipindi vyetu na tumekuja na mkakati mpya wa kuendelea kuwapatia burudani na habari zenye uhakika zaidi kama ilivyokuwa ada yetu,ninachowasihi ni kuendelea kusikiliza Magic FM kwa popote pale ulipo kupitia frequency zetu katika mikoa ambayo tunapatikana lakini pia kwa wale ambao mpo nje ya Tanzania kupitia tune in mnatupata ukiwa eneo lolote duniani,” alisema Kawau.
Miongoni mwa vipindi vilivyofanyiwa marekebisho ni kipindi cha Morning Magic kinachorushwa kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa nne, na kipindi kinachoruka kuanzia sa kumi mpaka saa kumi na mbili, pamoja na kile cha michezo na Magic kinachorushwa saa 2 mpaka saa 3 usiku.

Wimbo ‘Salome’ wa Diamond wamkuna Wema Sepetu, Diamond atia neno

Wema-7

Malkia wa filamu Wema Sepetu amekunwa na wimbo mpya wa Diamond Platnumz ‘Salome’ na kuamua kujirekodi video huku akiimba wimbo huo
Diamond alipost video instagram inayomwonyesha mwigizaji huyo akiimba wimbo ‘Salome’ huku akiandika ujumbe wa kuonyesha kufurahishwa na kitendo hicho.
“Hivi huku patakuwa ni kupatwa kwa nini?. Tisha sana ‘Salome’ wake Idris Sultan full Video link in my BIO and @rayvanny Bio,” aliandika Diamond kupitia instagram.
Hatua hiyo huwenda ikafungua njia zaidi kwa wawili hao kuaidia katika mambo yao.

23 Sep 2016

Jokate: Bado nafanya muziki, ila nahitaji menejimenti


14374059_178671149206962_327093865_n

Mwanamitindo na mwanamuziki nchini Tanzania, Jokate Mwegelo ambaye amekuwa kimya katika masuala ya muziki kutokana na kuwa busy na biashara, amesema bado anafanya muziki

Jokate ambaye wimbo wake wa mwisho kuutoa ulikuwa ‘Leo Leo’ aliomshirikisha Ice Prince kutoka Nigeria, alikuwa akihojiwa Ijumaa hii kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.
“Muziki bado nafanya ila bado nahitaji menejimenti ambayo ipo vizuri,” alisema. “Sitaki kufanya muziki niwe kama najaribu, nahitaji kuwa na timu ambayo tutafanya kazi ya serious kama ilivyo kwenye brand ya Kidoti. Bado natafuta timu ambayo itanisimamia katika muziki vizuri, sijaacha nimesimama tu hadi hapo nikapopata menejimenti nzuri,” alisema Jokate.

Utani wa Idris Sultan kwa Diamond na Zari

hereni
Kama huwezi utani basi jiweke mbali na Idris Sultan kwa kuwa ipo siku unaweza kujikuta ukifanya kitu usichokitarajia.
Mchekeshaji huyo ameandika ujumbe wa utani kwa Diamond na Zari kwenye mtandao wake wa Instagram baada ya hivi karibuni kusambaa kwa taarifa kuwa First Lady huyo wa WCB alikuta hereni kwenye chumba cha Diamond ikionekana kuwa alimsaliti na mwanamke mwingine.
“Ndio imeingia na DHL @diamondplatnumz nakupitishia hapo maana umepoteza control mambo yanamwagika hovyo mara hereni ulizisimamia kama kangaroo,” ameandika Idris kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo.
Hakuishia hapo Idris amempongeza Zari The Bosslady kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuweka picha ya hereni kwenye mtandao huo na kuandika ujumbe unaosomeka, “Happy birthday @zarithebosslady ðŸ˜….”

Staa wa Nigeria Chinedu Ikedieze (Aki) aisifia ‘Salome’ ya Diamond ‘I am a big fan’

chinedu-1

Salome ya Diamond Platnumz inaelekea kumshangaza staa huyo kwa mafanikio makubwa inayoendelea kuyakusanya
Baada ya video yake kuvutia views milioni 1 ndani ya siku mbili tu tangu itoke, wimbo huyo umeyagusa masikio ya mtu maarufu kwenye filamu za Nigeria, Chinedu Ikedieze anayejulikana zaidi kama Aki kwenye filamu zake
Akicomment kwenye post ya Diamond Instagram, Ikedieze amesema kuwa haelewi kinachoimbwa kwenye wimbo huo lakini ameupenda na kwamba ni shabiki wake mkubwa.
cs-oiyxgaa7hye
chinedu
Aki na Ukwa wamekuwa na mashabiki wengi Afrika nzima kwa filamu zao za comedy.

Kama unamtaka King Crazy GK kwenye show jipange, chini ya milioni 30 hafanyi show

jumaclick-blog
Msanii wa hip hop aliyewai kufanya vizuri na Kundi la East Coast Team, King Crazy GK amesema kwa sasa hafanyi show chini ya Tsh milioni 30.
Rapper huyo amedai hawezekani msanii kutoka nje alipwe zaidi ya Tsh milioni 100 alafu msanii wa ndani alipwe chini ya milioni 30.
“Kwa sasa mtu yeyote anayetaka kufanya kazi na mimi lazima awe amejikamilisha,” GK alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Kwa sababu ukiangalia wasanii wanaotoka nje ya Tanzania wakija huku wanalipwa hadi milioni 100, lakini sisi wa ndani hela inakuwa ndogo naamini tunaweza na muziki tunaofanya ni mzuri media zikiendelea kusapoti naamini hata sisi tuna uwezo wa kulipwa hela hizo,”
Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mzuri Pesa amesema kwa sasa mtu yeyote anayetaka kufanya naye kazi lazima awe amejipanga.

Fid Q: Nisingekuwa rapper, ningependa kuwa profesa wa chuo kikuu

fid-q
Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q amefunguka kwa kuitaja kazi aliyotamani kuifanya kama asingekuwa mwanamuziki.
Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Dj Show cha Radio One, Nico Track, rapper huyo amedai kuwa angekuwa ni mkufunzi wa chuo kikuu.
“Hamna kazi ninge-enjoy kuifanya kama ningekuwa Professa wa chuo kikuu, sijawahi kutaka kuwa daktari, rubani, mwanasheria wala yeyote,” amesema Fid Q.
“Mimi nimekuwa mtu wa kupenda vitu vya academy na vitu vingine vya masuala ya uelimishaji ndio maana hata kwenye muziki sifanyi Entertainment mimi nafanya Edutainment. Kwahiyo mimi ni Edutainer si Entertainer,” ameongeza.
Fid Q ni mmoja kati ya wasanii wenye uwezo wa kuchana na kuandika mistari yenye misamiati ambayo ndani yake imebeba ujumbe mzito.

Birthday ya Zari yaingia na neema, Diamond aonyesha nyumba ya familia aliyonunua SA

dai
Mkali wa muziki anayefanya vizuri na wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz Alhamisi hii siku moja kabla ya birthday ya mama watoto wake Zari, ameonyesha nyumba ya familia aliyonunua Afrika Kusini.
Muimbaji huyo ambaye ni mmoja kati ya wasanii wachache wenye mafanikio makubwa hapa nchini, hakuweka wazi nyumba hiyo imegharimu kiasi gani kuinunua.
“Wanakazana kujisifu matajiri Ilhali watoto zao wanaishi kwenye Nyumba zakupanga. Halafu leo yule yule wanaemtukana kutwa kwenye mitandao kuwa masikini, kajawa na shida, Kanunua nyumba kulekule kwao ili watoto wao waishi maisha bora kama wanayoyatamani. Heri ya siku ya Kuzaliwa Mama tee wangu. Nakupenda sana na unalifahamu hilo, natumai umeipenda nyumba yetu hii mpya South Africa. Nasubiria kwa hamu kusheherekea nawe siku yako hii kubwa kesho (leo) Zanzibar,” Diamond aliandika instagram.
Muimbaji huo amevunja zile tetesi za kwamba huwenda hayupo sawa na mama Tiffah baada ya mrembo huyo siku chache zilizopita kudai amekuta hereni za mwanamke mwingine chumbani kwake