Mwana FA amewataja Bill Nas na Darassa, kuwa ndio rapper wa kizazi cha sasa anaowakubali zaidi.
Amewataja Jumatano hii wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Campus Vibes cha Times FM.
“Bill Nas, Bill Nenga yupo hapo yaani without a doubt hata ukiniamsha saa nane usiku,” alisema Mwana FA. “Amepatia, muziki wake anavyotaka uwe ndio umekuja hivyo na wananchi wamemuelewa.”
FA anasema yeye ndiye aliyeanza kumtambulisha Nas kwa watu wa habari na anafurahi kuona kuwa amefahamika tayari na watu wanakubali muziki wake.
“Kafanya juhudi nyingi sana, namjua,” alisisitiza FA.
Pia rapper huyo mkongwe anaamini Darassa ni rapper wa moto ambaye huu ni wakati wake. “Darassa yuko vizuri sana nafikiri na yeye kahangaika sana na ameupatia sasa hivi.”
Kwa upande mwingine FA aliwataja rappers watano anaowakubali zaidi kwa muda kuwa ni Hashim Dogo, Profesa Jay, Fid Q, Jay Moe na Solo Thang.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni