Hatimaye wasanii wawili mapacha wanaounda kundi la P-Square, Peter na Paul Okoye wameshoot video ya wimbo wao mpya kwa mara ya kwanza tangu walipotengana na kila mtu kufanya kazi kivyake.
Wiki kadhaa zilizopita wasanii hao walitangaza kuungana tena na waliingia studio kutayarisha wimbo wao mpya ‘Bank Alert’ na wiki iliyopita walianza kushoot video hiyo.
Kupitia mtandao wa Instagram, Peter ameweka baadhi ya picha zinazowaonyesha wakiwa location kwa ajili ya kushoot video yao hiyo mpya na kuandika, “#Onset PSQUARE New Video Loading….. #Psquare4Life #BankAlert @rudeboypsquare @judeengees.”
“This time we took it to da street #PsquaresNewVideo #BankAlert Loading…..,” ameandika kwenye picha nyingine aliyoiweka kwenye mtandao huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni